Rachuonyo Duncan

Duncan Rachuonyo (Kaka D) ni mtangazaji wa KBC Redio Taifa, amewahi kukifanya Kipindi cha ‘Jabulani Afrika na Vuvuzela kila wiki usiku.

Anasomea utangazaji katika Chuo Kikuu cha Moi (Shahada) na ana stashahada kutoka Chuo A�Anwai cha Mombasa.

Rachuonyo amefanya kazi kama Mwandishi wa Kiswahili na Kampuni ya Nation Media Group (Taifa Leo – Daily Metro) na Radio Africa Group(Star Newspapers). Pia amefanya kazi akiwa mtangazaji wa Kiswahili katika kituo cha STAR FM, na ana tajriba ya utangazaji na uandishi wa zaidi ya miaka mitano.