PSC yakaribisha maombi ya waakilishi wake kwenye tume ya kuratibu mishahara, SRC

Tume ya kuwaajiri wafanyakazi wa umma-PSC imewahimiza wale wanaotaka kuiwakilisha katika tume ya kuratibu na kuwianisha mishahara-SRC kutuma maombi. PSC ambayo ni moja ya asasi 13 zilizo na nafasi katika tume ya SRC imewahimiza wale wanaotimiza masharti na kanuni zinazohitajika kutuma maombi yao pamoja na stakabadhi zinazohusianaA�A�kabla ya tarehe 6 mwezi ujao wa februari .Majina ya wale wote watakaorodheshwa kuhojiwa yatachapishwa kwenye tovuti ya tume hiyo.Tume ya huduma za bunge na bunge la seneti tayari zimeanzisha utaratibu wa kuwachagua waakilishi wake kuambatana na kifungu cha 230 cha katiba.Watakaoteuliwa sharti wawe na shahada kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa hapa nchini,ufahamu na ujuzi wa angalau miaka 10 katika maswala ya fedha na usimamizi,uchumi na sheria za wafanyakazi miongoni mwa mahitimu mengine,kando na kutimiza masharti ya sura ya sita ya katiba