Pombe husababisha asilimia 25 ya vifo Kenya

Takriban asilimia 25 yaA� vifo vyoteA� hapa nchini ni kutokana na unywaji pombe . Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya , mkurugenzi wa huduma za matibabu katika wizara ya afya Dkt . Jackson Kioko alisema ipo haja ya kutoa uhamasisho dhidiA� ya matumizi ya dawa za kulevya kote ulimwenguni . Dkt . Kioko hata hivyo alithibitisha kuwa wizara ya afya inaweka mikakati ya kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazozuia vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya hapa nchini .A� Alitoa wito kwa washirika wa maendeleo na wadau muhimu kuhakikisha kuwa kuna utekelezaji bora wa mikakati na sera za kuthibiti matumizi ya dawa za kulevya na kuongeza kuwa hii itasaidia kuimarisha ukuaji wa kiuchumi na kijamii kwa wale walioathirika .

Kulingana na ripoti ya mwaka 2017 ya matumizi ya dawa za kulevya duniani iliyotolewa na afisi ya umoja wa mataifa kuhusiana na dawa za kulevya na uhalifu (UNODC), zaidi ya robo bilioni ya watu kote ulimwenguni walitumia dawa za kulevya mnamo mwaka 2015.