Pombe haramu yapatikana Matuati kaunti ya Meru

Shirika la kukabiliana na bidaha ghushiA� (ACA) limepata pombe haramu katika boma moja huko Mutuati,A� kaunti ya Meru . Maafisa wa shirika hilo kwa ushirikiano na polisi pia wamekamata watu sita na bidhaa za pombe za thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40 na alama ghushi za halmashauri ya ukusanyaji ushuru hapa nchini.A� Kulingana na msimamizi wa utekelezaji wa shughuli za shirika hiloA� Lindsay Kipkemoi washukiwa hao walikuwa wakitengeneza aina mbali mbali za pombe ghushi , kuzipakia na kuwauzia watu wasiofahamu hasa katika kaunti za Meru, Isiolo naA� Laikipia . Wakati wa uvamizi huo maafisa wa shirika hilo walipata chupa zilizotumika kwenye maguni , vifuniko vya chupa , ala ghushi za shirika la kutathmini ubora wa biodhaa hapa nchini , alama za kampuni tano na zaidi ya lita 5000 za bidhaa inayoshukiwa kuwa pombe. Washukiwa hao walikamatwa na maghala yao kukaguliwa katika juhudi za kutafuta bidhaa haramu baada ya maafisa kupashwa habari na watengenezaji wa halali wa pombe hiyo. Hata hivyo mmiliki wa boma hilo alitoroka kabla ya uvamizi huo.