Polisi yaonya raia dhidi ya kuvuruga shughuli za IEBC

Polisi imewaonya wananchi dhidi ya kuwahangaisha, kuwatisha au kuhusika katika visa vyovyote haramu dhidi A�ya maafisa wa uchaguzi ikisema vitendo hivyo ni kinyume cha sheria za A�uchaguzi. A�Kwenye taarifa, msemaji wa polisi George Kinoti, alisema polisi wameagizwa kuchukua hatua kali dhidi ya watu au makundi A�yanayovurugha au kuwazua maafisa wa Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka kutekeleza kazi zao halali.A� A�Kuhusiana na visa vilivyotokea Awasi, Kaunti ya A�Kisumu na A�Bondo A�na Gem A�katika Kaunti ya Siaya A�ambapo maafisa wa Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka walishambulia na watu waliokuwa na pikipiki kisha wa wakawajeruhi, Kinoti A�alisema polisi waliweza kuwanurusu maafisa hao na A�sasa uchunguzi unaendelea kuwakamata waliohusika. Mjini A�Kisumu, kisa hicho kilitokea huku maafisa waliokodishwa A�kuendesha A�uchaguzi A�walipokuwa wakikusanyika kwenye A�ukumbi wa A�Awasi Multicultural Christian A�Centre kwa mafunzo A�ya siku nne. A�Afisa Mkuu wa uchaguzi, Kaunti ya Kisumu, John Ngutahi, alisema kikao hicho kilikuwa kinaendelea ili kuwaandaa maafisa 399 wa kusimamia uchaguzi na manaibu waoA� A�uvamizi huo ulipotokea. Washambualiaji hao walidai kuwa mafunzo hayo hayakuwa halali.