Polisi wavamia nyumba ya mfanyibiashara Jimmy Wanjigi

Polisi wamevamia nyumbani kwa mfanyabiashara mashuhuri Jimmy Wanjigi katika mtaa wa Muthaiga jijini Nairobi. Kundi la maafisa kutoka kikosi Maalum cha kukabiliana na Uhalifu kilivamia nyumbaniA�A� kwa WanjigiA� jana alasiri. Haijulikani sababu ya uvamizi huo lakini kuna tuhuma kuwa unatokana na kisa cha bunduki kupatikana kwenye jengo moja mjini Mombasa. Maafisa wa usalama kwenye kaunti ndogo ya Malindi walivamia jengo linaloaminika kumilikiwa naA� WanjigiA� na wakapataA� bunduki tano aina ya AK 47 na risasi 93A� pamoja na fuvu la kasa. Shughuili hiyo ilihusisha maafisa wa usalama kutoka vikosi tofauti ambao walifika kwenye jengo hilo wakiwa na agizo la Mahakama kuipekua.A� Maafisa hao waliwatia nguvuni wafanyakazi wanne ambao wamezuliwa kwenye kituo cha polisi cha Malindi ili wahojiwe. Afisa mkuu wa polisi kwenye kaunti ndogo ya Malindi Matawa Muchangi amesema wameanza uchunguzi kutambua mwenye bunduki hizo na sababu ya kuzimiliki.