Polisi Watoa Zawadi Ya Milioni 2 kwa kurepoti Gaidi

Polisi wametoa picha za washukiwa watatu wa ugaidi wanaohusishwa na mashambulizi dhidi ya mabasi katika maeneo ya Mandera na Elwak. Polisi wameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni 2 kwa yeyote atakayewasilisha habari kuwahusu na kuhimiza yeyote aliye na habari kuwahusu kupiga ripoti kwa kituo cha polisi kilichoko karibu .

Mshukiwa wa kwanza Abdullahi Issak Diyat anatakikana kwa kuhusika na shambulizi la mwezi Novemba mwaka 2014 dhidi ya basi moja la Makkah lililosababisha vifo vya wakenya 28 wasiokuwa na hatia . Pia anatakikana kwa mauaji ya mwezi desemba mwaka 2014 ya wafanyikazi wa migodi huko Mandera .

Mshukiwa mwengine , Idriss Issack Ismail, anatakikana kwa mashambulizi sawia na ya Diyat.

Ahmed Uweys, ambaye ni mshukiwa wa mwisho anasemekana kujiunga na kundi la Al-Shabaab kama mpiganaji kabla ya kujiunga na kitengo cha Amniyat cha kundi la al-shaabab. Rekodi za polisi pia zinamhusisha na mashambulizi katika mgodi wa Mandera na katika basi la Makkah. Polisi wamewahimiza wakenya kuwa macho huku akionya kuwa washukiwa hao wanaaminika kuwa wamejihami na hatari.