Polisi Waliohusishwa Na Mauaji Ya Wakili Willie Kimani, Wafikishwa Mahakamani

Polisi watatu wa utawala waliohusishwa katika mauaji ya wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa teksi walifikishwa katika mahakama moja ya Nairobi leo asubuhi. Hata hivyo, sajenti mkuu,A�Fredrick Leliman, kopilo Stephen Chebulet na konstebo Silvia Wanjiku watazuiliwa kwa siku-14 kuruhusu maafisa wa upelelezi kukamilisha uchunguzi wao. Hakimu mkuu. Daniel Ogembo alikubali ombi la mkurugenzi wa mashtaka ya umma la kuwazulia maafisa hao watatu. Katika ombi lake, mkurugenzi wa mashtaka, alisema maafisa wa upelelezi hawajakamilisha uchunguzi wao kwani washukiwa hao walikamatwa siku ya ijumaa. Alisema miili hiyo haijafanyiwa uchunguzi na pia maafisa wa upelelezi wanaendelea kukusanya ushahidi. Wakili Cliff Ombeta aliyejitolea kuwakilisha washukiwa hao watatu hakupinga ombi la mkurugenzi wa mashtaka ya umma. Kesi hiyo itatajwa tarehe-18 mwezi huu.