Polisi Wanasa Pembe Za Ndovu Za Thamani Ya Milioni 6.4 Katika Uwanja Wa JKIA

Maafisa wa polisi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wamenasa mzigo uliokuwa na vipande vya pembe za ndovu vya thamani ya shilingi milioni-6.4. Mzigo huo ulikuwa ulisafirishwa kutoka mjini Maputo nchini Msumbiji kuelekea Bangkok, Thailand. Kulingana na maafisa wa polisi, vipande hivyo vya pembe za ndovu vilikuwa vimefichwa kamaA�mawe ya thamani. Polisi walisema vipande hivyo-18 viligunduliwa wakati mzigo huo ulipokuwa ukikaguliwa. Afisa mkuu wa upelelezi katika uwanja huo wa ndege, Joseph Ngisa alisema serikali ya Msumbiji imefahamishwa kuhusu kisa hicho na kuitaka kufwatilia swala hilo. Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hiki cha ulanguzi