Polisi Wamtia Nguvuni Mgombea Urais Kizza Besigye

Mgombea urais wa chama cha upinzani cha FDC nchini Uganda Kizza Besigye alikamatwa na kuzuiliwa kwa muda na maafisa wa polisi mjini Kampala. Polisi walitumia vitoaA� machozi kuwatawanya wafuasi wakeA� na wakamkamata mwanasiasa huyo.Alizuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi cha Kira Road na kuaachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka.Polisi walisema alikamatwa kwaA� kutatiza uchukuzi mjini. Besigye alikua afanye mikutano ya kampeni katika mji mkuu Kampala. Mkuu wa Polisi Jenerali Uganda Kalekezi Kayihura amethibitisha kwamba polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani lakini akakanusha habari kwamba Bw Besigye alikamatwa.
Maafisa wengine wa polisi walisema kiongozi huyo wa upinzani alizuiliwa tu kwa muda.Leo ilikua mara ya kwanza kukamatwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka huu.Uchaguzi huo utafanyika Alhamisi.