Polisi Wamkamata Mwanamke Anayetuhumiwa Kumuua Babake Kakamega

Polisi huko Kakamega wamemtia nguvuni mwanamke mmoja ambaye yadaiwa alimuua babake kwa kumkata kwa panga na kuwajeruhi vibaya watu wengine sita kutoka familia yake. Kilichosababisha Raphael Amboso mwenye umri wa miaka 40 kuwashambulia jamaa zake hakijabainika. Waliojeruhiwa wanapokea matibabu katika hospitali ya misheni ya Mukumu, huku mwanamke huyo akijasalimisha mwenyewe kwa polisi baada ya kutekeleza unyama huo. Naibu wa kamisha wa A�kaunti anayesimamia sehemu hiyo Dorcas Rono amesema mshukiwa atafikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kitendo hicho. Mbunge wa shehemu hiyo Silverse Anami A�amesema mwanamke huyo anashukiwa kuwa mwanachama wa genge moja la wahalifu lenye makao yake huko Mombasa. Amboso kwa wakati huu yuko kwenye korokoro za polisi huku uchunguzi kuhusiana na kitendo kilichowashangaza wakazi ukiendelea. Mnamo mwaka uliopita mwanake huyo alijaribu kujitoa uhai lakini akanusuriwa na wanakijiji.