Polisi Wachunguza Njama Ya Ulanguzi Wa Binadamu

Maafisa wa polisi wanachunguza njama ya ulanguzi wa binadamu baada ya kukamatwa kwa raia-13 wa Ethiopia kwenye mpaka baina ya Kenya na Tanzania. Kundi hilo lilikamatwa Jumapili usiku katika eneo la Lunga Lunga, kaunti ya Kwale. Afisa mkuu wa polisi huko Msabweni Joseph Omija alisema njama hiyo inahusisha usafirishaji wa kimagendo wa raia wa kigeni hadi nchini Afrika kusini. Raia wengine-23 wa Ethiopia walikamatwa mwezi uliopita baada ya kuviziwa katika nyumba moja mtaani Kahawa West, jijini Nairobi. Afisa huyo wa polisi alisema inaaminika kuwa raia hao walikuwa njiani kwenda Afrika Kusini lakini lengo lao halikujulikana mara moja kwaniA� hawazungumzi kiingereza.