Polisi Wa Trafiki Kusajiliwa Kakamega

trafik
Jumla ya polisi-134 wa trafiki kutoka magharibi ya Kenya watasajiliwa na tume ya kitaifa ya huduma za polisi mjini Kakamega. Akiongea alipomtembelea mrakibu wa eneo la magharibi afisini mwake, mwenyekiti wa tume hiyo Johnston Kavuludi alisema shughuli hiyo ya wiki moja itahusisha maafisa wa polisi wa ngazi zote katika eneo hilo.

Kavuludi alisema usaili huo utatilia mkazo idara ya polisi wa trafiki kutokana na utendkazi wao unaowafanya kutangamana na wananchi mara kwa mara. Usaili huo utalenga masuala ya uadilifu, kifedha na viwango vya elimu vinavyohitajika kujiunga na kikosi cha polisi. Wale watakaopatikana kuwa hawastahili kuhudumu katika kikosi cha polisi huenda wakaachishwa kazi au kuchukuliwa hatua za kisheria.