Polisi nchini Brazil wakamata walanguzi wa dawa za kulevya

Polisi nchini Brazil wamemkamata mshukiwa mmoja anayeaminika kuwa kiongozi wa genge la walanguzi wa dawa za kulevya nchini Mexico. Kwa Kwa mujibu wa kibali cha kukamatwa kwake, polisi walimzuilia Jose Gonzalez Valencia mwenye umri wa miaka 42 ambaye anasemekana kuwa kiongozi wa kundi la Jalisco New Generation Cartel ili kutimiza ombi la marekani la kumrejesha makwao. Genge hilo linasemekana kukuwa na kupanuka katika miaka ya hivi maajuzi na kutoa upinzani kwa kundi la Sinaloa ambalo kiongozi wake Joaquin a�?El Chapoa�? Guzman alikamatwa kwa kuhusika na biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Mexico.