Polisi 18 wauawa kwenye shambulizi la Islamic State, Misri

TakribanA� polisi 18 wameuawa kwenye shambulizi la wanamgambo wa Islamic state dhidi yaA� msafara wa walinda usalama katika eneo la Sinai, nchini Misri. Kwa mujibu wa vyombo vya usalamaA� wanamgambo hao walilipua bomu la kutegwa ardhini karibu na mji wa El-Arish na kuharibu magari matatu ya deraya na la nne lililokuwa na mitambo ya kuvuruga mawasiliano ya adui. Wanamgambo hao walitumia bunduki za rashasha na kuwauwa walinzi waliokuwa wamenusurika shambulizi hilo. Wizara ya mashauri ya ndani ilithibitisha kutokea kwa shambulizi hilo. Mamia ya walinda usalama na wanajeshi wameuawa naA� wanamgambo wa kundi la Islamic state na washirika wao tangu mwaka wa 2013, wakati wanajeshi walipopindua serikali ya rais Mohamed Morsi.