Pizza Yagharimu Elfu 73

Kwa muda mrefu Pizza imechukuliwa kuwa chakula cha bei nafuu hasa katika nchi za magharibi, lakini sasa kampuni moja jijini London inanuia kubadili hali hiyo kwa kutengeneza pizza inayogharimu pauni 500 au shilingi elfu-73 za Kenya. Kampuni ya Pizza GoGo inawauzia wateja pizza hiyo kwa bei sawa na kipakatalishi au tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi jijini New York. Pizza hiyo inapatikana kwenye matawi 15 ya kampuni hiyo jijini London lakini ni sharti wateja watoe ilani ya siku tatu.

 

malimwengu