Pigo Kwa Desert Foxes Baada Ya Saphir Taider Kujeruhiwa Kabla Ya AFCON

Timu ya  Desert Foxes ya Aljeria imepata pigo kubwa baada ya kiungo wa kilabu cha Bologna cha Italia  Saphir Taider  kujeruhiwa kinena Jumatano hii wakati wa mazoezi  muda mfupi kabla ya timu hiyo kuondoka kwenda  Franceville nchini  Gabon  kushiriki katika fainali za kombe la bara Afrika. Kulingana na shirikisho la soka nchini Aljeria, Taider aligongana na mwenzake wakati wa mazoezi na madaktari wa timu hiyo wametangaza kuwa  jeraha hilo haliwezi kumruhusu kushiriki katika fainali hizo. Taarifa rasmi kutoka kwa shirikisho la soka nchini humu lilifichua kuwa  nafasi ya kiungo huyo itajazwa na mchezaji mwengine ambaye bado hajatajwa. Aljeria iko kundi ‘B’  pamoja na Tunisia, Senegal na  Zimbabwe.  Timu hiyo itafungua kampeini zao Jumapili hii dhidi ya Zimbabwe  mjini  Franceville.