Pierre-Emerick kusalia katika timu hiyo hadi mwaka 2021

Mshambulizi wa kilabu cha Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang amezidisha muda wa kandarasi yake na atasalia katika timu hiyo hadi mwaka 2021.Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 28 alikuwa mchezaji mfungaji mabao mengi nchini Ujerumani msimu uliopita kwa jumla ya mabao 31, bao moja zaidi ya Robert Lewandowski wa Bayern Munich. Aidha Aubameyang amefunga mabao 13 katika mechi 15 alizocheza msimu huu. Kandarasi yake ya awali ilipaswa kukamilika mwezi Juni mwaka 2020. Aubameyang, aliyezaliwa nchini Ufaransa, alijiunga na Dortmund mwaka 2013 kutoka Saint-Etienne. Alianza kucheza soka ya kulipwa katika kilabu cha Milan na hatimaye kuvichezea vilabu vinne vingine kwa mkopo kabla ya kujiunga na Saint-A�tienne kwa muda mrefu mwaka 2011. Baada ya kutwaa kombe la a�?Coupe de la Liguea�� mwaka 2013, Aubameyang alijiunga na Dortmund na kuisaidia kutwaa ubingwa wa kombe la a�?DFL-Supercupa�� mara mbili katika miaka ya 2013 na 2014. Aubameyang alichaguliwa mchezaji bora wa Afrika mwaka 2015, huku akiwa mzaliwa wa kwanza wa Gabon kupokea tuzo hiyo.