Philomena Mwilu apokea kesi ya kupinga kuchaguliwa kwa rais Uhuru

Kesi ya kupinga kuchaguliwa tena kwa Rais Uhuru Kenyatta iliyowasilishwa mahakamani na mwanaharakati Okiya Omtata imewasilishwa kwa Naibu wa Jaji mkuu Philemona Mwilu kubuni jopo litakalosikiza kesi hiyo. Na sajili wa mahakama ya juu Daniel Ole Keluwa alisema pande zote zinazohusika katika kesi hiyo zimezingatia maagizo ya mahakama na kuwasilisha ushahidi wao. Rais Uhuru Kenyatta, mwanasheria mkuu Githu Muigai na Tume ya IEBC wanapinga kesi hiyo ya upinzani wakisema mahakama ya juu haina uwezo wa kuzikiza na kuamua kesi hiyo. Wanataka kesi hiyo itupiliwe mbali. A�Omtata aliwasilisha kesi ya kutaka IEBC izuiwe kumtangaza Uhuru kuwa rais mteule kufuatia kujiondoa kwa Raila Odonga kwenye uchaguzi mpya wa urais uliofanyika Oktoba 26. Alidai kwamba uchaguzi huo si halali kwa vile hakukufanyika uteuzi wa wagombea.