Philip Kinisu, Ashinikizwa Kujiuzulu Ili Kuruhusu Uchunguzi Kufanywa

Mwenyekiti wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi-EACC anayekumbwa na zogo, ucPhilip Kinisu, ametakiwa kujiuzulu kwa hiari ili kuruhusu hunguzi kufanywa kuhusu shughuli za kampuni yake na shirika la huduma ya vijana kwa taifa a��NYS. Kwenye barua kwa mwanasheria mkuu, makamishna wanne wa tume ya kupambana na ufisadi na afisa mkuu wa tume hiyo Halakhe Waqo, wanamtaka Kinisu kuwajibika binafsi bila kusimamishwa kazi chini ya kifungu cha 47 sehemu ya 7 ya sheria kuhusu uongozi na maadili.Makamishna hao; Sophia Lepuchirit, Dkt. Dabar Abdi Maalim, Paul Mwaniki Gachoka na Rose Mghoi, wanasema ikitiliwa maanani wadhifa ambao Kinisu anashikilia na uhusiano wake na kampuni ya Esaki Limited ambayo inahusishwa na shughuli za kushukiwa na shirika la NYS, maslahi ya kibinafsi ya mwenyekiti huyo wa tume ya kupambana na ufisadi yanakinzana na maslahi ya umma. Kampuni ya Esaki Limited inalaumiwa kwa kupokea zabuni za shilingi milioni 34.5 kwa uuzaji vifaa mbali mbali kwa shirika la NYS kati ya mwezi Oktoba mwaka wa 2014 na mwezi Novemba mwaka wa 2015. Inadaiwa kwamba kampuni ya Esaki Limited pia ilikabidhiwa kwa pupa zabuni ya uwasilishaji dawa za kuthibiti ugonjwa wa Malaria licha ya kupewa leseni ya ununuzi dawa za waduu waharibifu siku moja kabla ya zabuni hiyo kuolewa na baada ya zabuni hiyo kufungwa, madai ambayo Kinisu ameyakanusha kwa dhati.