Pep Guardiola aeleza nia ya kufikisha Manchester City kwenye fainali ya clubu bingwa barani ulaya

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola  amesema kuwa nia yake ni kuifuzisha timu hiyo awamu ya robo fainali ya kinyan’ganyiro cha ligi ya mabingwa barani Ulaya  huku akisema kuwa hana uhakika ikiwa timu hiyo ina uwezo wa kulitwaa kombe hilo msimu huu.

City imetia fora msimu huu huku ikiongoza msururui wa ligi kuu Uingereza alama 16 zaidi ya wapinzani wao wa karibu. City ingali inawania ubingwa wa kombe la FA.

Aidha City imefuzu kwa fainali ya kombe la Carabao itakayoandaliwa baadaye mwezi huu. Hata hivo, City imefuzu kwa awamu ya  nusu fainali ya ligi ya mabingwa mara moja pekee, msimu wa mwaka 2015/2016 chini ya ukufunzi wa Manuel Pellegrini. Aidha ilibanduliwa mashindanoni katika raundi ya kumi na sita bora msimu uliopita na  Monaco katika kampeni ya kwanza kwa kocha Pep Guardiola akiwa mkufunzi wa timu hiyo katika kipute hicho cha bara ulaya. Wakati uo huo Guardiola amedokeza kuwa huenda mchezaji Leroy Sane akashiriki mechi ya leo usiku dhidi ya Basel.