Pendekezo la China la Mkanda Mmoja Njia Moja litanufaisha Kenya na Afrika kwa Jumla

Na Eric Biegon, Beijing.A�

Rais wa China Xi Jinping alipendekeza na kukuza mpango wa mkanda mmoja njia moja (One Belt One Road) miaka 3 iliyopita, akiutangaza kama kielelezo mpya ya ushirikiano ambayo itachochea maendeleo ya pamoja na mafanikio.

Dhahiri, hii imekuwa kipengele muhimu zaidi ya sera za kigeni ya China.A�Wengi wanautambua kama mchango wa China kwa utaratibu mpya wa dunia.

Mpango huu hasa unalenga kuunganisha nchi za Afrika, Ulaya na bara Asia kupitia mradi kabambe wa miundombinu, ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa.A�Nchi zinazoendelea ambazo zimejiunga katika dhana hii, kwa kiasi kikubwa zinaangalia hali zao za kiuchumi.

Mpango huu unaoongozwa na China imeshika kasi barani Afrika na ni rahisi kuona ni kwa nini.A�Hata ingawa bado inajihesabu kuwa taifa linaloendelea, mafanikio ya kiuchumi ya China ni mfano wa kuigwa na dunia.A�Uongozi wa China wenye makao makuu yake mjini Beijing unataraji kwamba mafanikio hii inaweza kuigwa hasa barani Afrika.

Kwa maoni ya rais Xi, mpango huu wa mkanda mmoja njia moja itatoa fursa kwa mataifa ya Afrika kuafikia uwezo wao wa maendeleo imara.A�Safari ya China kufikia mafanikio, kwa mfano, inaonekana chanzo chake kumetokana na kuunganishwa kwake ndani.

China ina maendeleo imara ya reli, barabara na miundombinu ya hewa kote nchini.A�China inajivunia maelfu na maelfu ya maili ya barabara za kasasa, zaidi kuliko nchi yoyote duniani.

Nchi hiyo ambayo ni kubwa zaidi kiuchumi barani Asia, imejenga mtandao wa reli wa kisasa kuunganisha maeneo yenye umbali wa maelfu ya maili.A�Nchi hiyo pia imefanya maendeleo ya viwanja vya ndege katika miaka 30 iliyopita.A�Ukitazama mkondo na hali hii, ni rahisi kusema, malengo mengi ya uchumi ya China imetokana na usafiri.

Mfano wa Kenya

Ndani ya Afrika, matunda ya Road & Belt tayari yanaonekana katika Kenya.A�Ujenzi wa reli ya kisasa, maarufu Standard Gauge Railway, wenye gharama ya shilling bilioni 327 na upanuzi wa bandari ya Mombasa imefanya nchi hiyo kuvutia makampuni ya kimataifa mengi ambayo wameonyesha hamu ya kuwekeza katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

SGR, ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwezi ujao, itaunganisha mji wa pwani wa Kenya ya Mombasa hadi mji mkuu wa Nairobi.A�Awamu ya pili ya SGR A�itaunganisha Nairobi hadi Naivasha, Kisumu, Malaba kisha Uganda, Rwanda na South Sudan.

Bandari ya Lamu ni mradi mwingine ambayo inajengwa na China.A�Mara baada ya kukamilika, bandari hiyo itaunganisha Sudan Kusini na Ethiopia.

Wataalam wa Kiuchumi wanashikilia mtazamo kwamba hii itazua uwezekano wa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kuongezeka kwa Kenya na nchi zote zinazohusika.

Kwa maoni yao, vituo vya biashara vitachipuka kando kando mwa reli hiyo.A�Katika mchakato huu, sekta ya chakula, mavazi, ujenzi na mafunzo kati ya mengine zitastawi.

Faida hizi huenda hazitaonekana kwa sasa lakini Rais Uhuru Kenyatta amepongeza mpango huo akisema itachochea ukuaji wa nchi hiyo katika mwaka 2030 na kuendelea.

“Lazima tuone uwekezaji mkubwa katika Reli kama uwekezaji unaostahili ili kuimarisha ajenda ya kikanda.A�Uchumi wa nchi utanawiri tu kukiwepo msingi wa miundo mbinu sahihi.” Alisema Rais Kenyatta

Ujenzi wa Viwanda Afrika

Ufanisi tele ambao umetokana na ujenzi wa hizo miundombinu ni jambo ambalo nchi zinazoendelea lazima ziangalie.

Umoja wa Afrika (AU), kufikia sasa imezindua ajenda 2063, ambayo inalenga kuharakisha kujengwa kwa viwanda vya kisasa Afrika.A�Waangalizi watadumisha kwamba A�Mpango wa Belt & Road utatoa nafasi ya kimkakati wa kuoanisha maendeleo ya China na maono hii ya Afrika.

Wataalam wa Kiuchumi wanashikilia maoni kwamba ukosefu wa kuunganishwa imekuwa kikwazo kubwa kwa ukuaji wa Afrika.A�Wote kama nchi binafsi na kama eneo, bara la Afrika haina miundombinu ya usafiri inayofaa.

“Afrika imejaliwa rasilimali tajiri asili.A�Bara hilo lina uwezo mkubwa.A�Lina uwezo wa kuanzisha viwanda vikubwa.A�Tatizo kubwa hata hivyo ni kwamba hata nchi jirani hazijaunganishwa.A�Usafirishaji ni kikwazo.” Alibainisha Profesa Wang Yiwei wa Chuo Kikuu cha Renmin mjini Beijing.

Kwa maoni yake, Afrika ina uwezo wa kupunguza kuongezeka kwa kina cha umaskini.A�Ili kukabiliana na hii, Prof Wang anasema nchi zinazoendelea za Afrika, mmoja mmoja na kwa pamoja lazima ziwekeze kwenye ujenzi wa viwanda.A�Hii anasema itasaidia Afrika kuongeza uwezo binafsi wa maendeleo.

Hata hivyo kufikia mchipuko wa viwanda, mwenzake kutoka Chuo kikuuu cha Tsinghua Profesa Kejin Zhao anasema serikali za Afrika lazima zikumbatie mfumo wa Mkanda Mmoja Njia Moja.

“Afrika inahitaji kuboresha miundombinu ya kanda yake, na kuwekeza katika mtandao salama ardhini, baharini na hewani, pamoja na kuinuaA� kuunganishwa kwao kufikia ngazi ya juu.” Anasema

Wasomi hao wawili wanasisitiza kuwa mradi wa Belt & Road kwa Afrika A�utaimarisha biashara na kuwezesha uwekezaji zaidi, kuanzisha mtandao wa maeneo ya biashara huru ili kukidhi viwango vya juu na kudumisha uhusiano wa karibu wa kiuchumi.A�Hii wanasema itakuwa itachangia kuleta mazingira mazuri ya uwekezaji.

Zaidi ya hayo, Wang na Zhao wanasema mpango huu utaimarisha ubadilishanaji wa utamaduni, kuhamasisha ustaarabu tofauti na kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kushamiri kwa pamoja.

Mfumo wa Ushirika A�

Katika moyo wa mfumo huu A�ni roho ya kugawana.A�China inaongoza katika suala hili.A�Kwa sasa, China inafanyia marekebisho na kuboresha muundo wake wa viwanda kwa kusafirisha nje shughuli za ziada za viwanda vyake.

Wachambuzi wa kiuchumi wanasema kuwa kutokana na kupanda kwa gharama ya kazi, kazi kubwa ya viwanda China ni kuhamisha baadhi ya viwanda yao kuelekea Afrika.A�Bara hilo laonekana kunufaika sana na mabadiliko haya.

Viwanda wa viatu na nguo Ethiopia, iliyobuniwa na kampuni ya Kichina ya Hujian Group, ni mfano halisi.A�Viwanda hivyo vimetengeneza nafasi za ajira kutokana na kwamba vimeajiri wenyeji zaidi ya watu 6,000.

Kundi la Hujian ambayo imewekeza sana nchini Ethiopia pia ilitia saini mkataba wa thamani ya bilioni 1.5 dola za Marekani kwa Nigeria ili kukuza kiwanda cha viatu katika jimbo la Abia.

Mwanzilishi wa kampuni hiyo bwana Zhang Huarong anasisitiza kwamba makampuni mengine mengi ya Kichina yana nia ya kuwekeza zaidi katika Afrika kwa muda mrefu kama hali ni nzuri.

Kenya, Rwanda na Tanzania ni nchi nyingine za Afrika, ambazo zinasemekana kutafuta makampuni kutoka China zitakazowekeza kwa sekta ya nguo kupitia mipango ya maendeleo ya hifadhi ya viwanda.

Prof Zhao anakadiria kwamba nchi kati ya tano (5) hadi kumi (10) za Afrika zitashushudia sekta zao za viwanda kuinuka zaidi ndani ya miaka mitano kutokana na kuhamishwa kwa viwanda kutoka Asia.

Kwa makusudi na madhumuni, mpango wa One Belt One Road inapania kueneza uwezeshaji wa uwekezaji wa biashara, kupunguza vikwazo vya uwekezaji wa A�biashara, kusukuma gharama ya chini ya uwekezaji katika biashara pamoja na kukuza ushirikiano wa kikanda wa kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama.

 

Isitoshe, waangalizi wanasema mfumo huu itafungua na kupanua Afrika kutokana na kwamba miongoni mwa mambo mengine, Belt & Road inataka kuunganisha nchi zisizo na bandari.

 

Kwamba China inaendelea kuwekeza Afrika sana si siri tena.A� Takwimu zinaonyesha kuwa mwishoni mwa mwaka 2015, makampuni ya Kichina yalikuwa yamewekeza biashara zaidi ya 3,000 katika bara hilo.A�Makampuni haya yametawanyika Kenya, Tanzania, Ethiopia, Afrika ya Kusini, DRC, Nigeria, Zambia, Sudan, Zimbabwe, Ghana, Mauritius na Angola.

 

Hizi makampuni zinahitaji mazingira mazuri ili kustawi na kunufaisha shughuli zao katika mataifa hayo.A�Ili kufanikisha hili, Afrika lazima ishughulikie vikwazo ambazo huzuia biashara.A�Muundo wa sasa wa Road & Belt inatoa njia halali na madhubuti ya kutatua tatizo hili.

 

Afrika inataka kuimarisha sekta ya viwanda kama njia ya kujipatia uhuru wa kiuchumi.A�Viwanda hata hivyo haviwezekani bila muunganisho.A�Kasi ni kiini na ni muhimu.A�Mfumo wa Mkanda Mmoja Njia Moja itasaidia bara la Afrika kufikia ndoto hii.