Paul Nkata ateuliwa kuwa kocha wa Uganda Revenue Authority

Mkufunzi Paul Nkata, raia wa Uganda, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Uganda Revenue Authority, mwezi mmoja baada ya kutimuliwa na timu ya ligi kuu ya Sportpesa, Bandari.

Haya yanajiri wiki moja baada ya Ibrahim Kirya na wasaidizi wake kutimuliwa kutoka timu hiyo inayoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Uganda.