Papa mtakatifu Francis kutembelea Myanmar na Bangladesh

Papa mtakatifu Francis ameondoka mji wa Vatican kuelekea nchini Myanmar katika ziara ya kwanza kuwahi kufanywa na papa mtakatifu katika taifa hilo ambalo mwaka huu limelaumiwa pakubwa mwaka huu kutokana na mauaji ya kikabila. Anatarajiwa kukutana na kiongozi wa taifa hilo Aung San Suu Kyi na kiongozi wa jeshi la taifa hilo. Ziara hiyo ilipangwa kabla ya mzozo ulioko wakati papa alipokutana na  Suu Kyi mjini Vatican mwezi Mei mwaka huu. Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya  Nobel amekabiliwa na shutuma kali kutokana na kimya chake kuhusiana na yanayoendelea nchini humo. Papa mtakatifu baadaye atazuru  Bangladesh na kukutana na kundi la wakimbizi wa kundi la  Rohingya. Zaidi ya watu laki sita wametorokea taifa jirani la Bangladesh tangu mwezi Agosti wakati mashambulizi dhidi ya vituo vya polisi yalipochochea msako wa kijeshi katika jimbo la  Rakhine tangu mwezi Agosti. Kundi kubwa la wakatoliki walio wachache wapatao laki sita wanatarajia kuhudhuria misa itakayoandaliwa na papa mtakatifu huko Yangon.