Mawakili Waliokiuka Maadili Kufichuliwa

Ofisi ya mwanasheria mkuu na idara ya haki imechapisha orodha ya mawakili waliochukuliwa hatua za nidhamu kwa kukiuka kanuni na maadili ya taaluma yao .Orodha ya mawakili hao 32 ilikabidhiwa kwa mwanasheria mkuu professa Githu Muigai wiki iliyopita na katibu wa tume ya kupokea malalamiko kuhusu mawakili James Marienga.Majina ya mawakili hao yanatarajiwa kuchapisha katika gazeti la serikali toleo la siku ya Ijuma tarehe 20 mwezi huu.Uamuzi wa kuchapisha majina hayo unafwatia ongezeko la malalamiko kuhusu visa ambapo mawakili wanawahadaa wateja wao,na kutia doa sifa ya taaluma hiyo.