Oparanya na Mutua wapendekeza kufanyiwa marekebisho mfumo wa serikali kuu nchini

Gavana wa kaunti ya Kakamega, Wycliffe Oparanya na mwenzake wa Machakos – Alfred Mutua, wamependekeza kufanyiwa marekebisho- mfumo wa serikali kuu nchini ili kujumuisha wadhifa wa waziri mkuu, ma-naibu wawili na kiongozi rasmi wa upinzani ili kuhakikisha kwamba pande zote zinawakilishwa serikalini. Wakiongea katika eneo-bunge la Shinyalu, kaunti ya Kakamega, ma-gavana hao walisema kwamba hatua hiyo itatoa nafasi kwa viongozi wengi zaidi kushirikishwa katika maswala ya serikali.

Wakati huo huo; viongozi hao wawili walipongeza mpango wa ushirikiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta A�na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.