Oparanya Amtaka Wetangula Kupuuza Rabsha Zilizotokea lli Kudumisha Amani

Gavana wa kaunti ya KakamegaA� Wycliffe Oparanya amemtaka kigogo mwenza wa muungano waA� CORDA� Moses Wetangula kupuuzaA� matukio yaliyokumba hafla ya uzinduzi wake wa kuwania urais katika juhudi za kudumisha muungano waA� CORD . Oparanya amesema rabsha zilizokumba hafla hiyo hazifai kuchukuliwa kwa uzito huku akipuzilia mbali madai kuwa rabsha hizo huenda zikasambaratisha muungano waA� CORD . Kulingana na A�Oparanya matukio yaliyotokea siku hiyo yanafaa kushtumiwa vikali kwani yanaleta dhana ya kutokuwa na umoja kwenye muungano wa CORD. Akiongea katika hafla ya kuchangisha pesa huko Malava, Oparanya alimtaka Wetangula kupuuza matukio hayo na kuendeleza azma yake ya kuwania urais wa nchi hii.