Omar al-Bashir atahudhuria mkutano Saudi Arabia

Rais wa Sudan Omar al-Bashir atahudhuria mkutano nchini A�Saudi ArabiaA� siku ya jumamosi na lakini hajapokea ishara kuwa atakutana na rais A�Donald Trump kwa mujibu wa waziri wa mashauri ya kigeni wa A�Sudan. Bashir anatafutwa na mahakama ya kimataifa kuhusu kesi za jinai-ICC kwa kuhusika na uhalifu wa kivita na huwa anaepukwa na viongozi wa mataifa ya magharibi. A�Ziara ya Trump nchini A�Saudi Arabia siku ya jumamosi ni yake ya kwanza ya kimataifa tangu achaguliwe kuwa rais. Anatarajiwa kuzuru mataifa ya Israel na bara ulaya.