Olivier Giroud hatashiriki katika mechi kati ya Arsenali na Liverpool

Olivier Giroud hatashiriki katika mechi ya ligi kuu nchini Uingereza kati ya Arsenali na Liverpool siku ya Ijumaa, baada ya kuumia katika ushindi wa Arsenali wa bao moja kwa sifuri dhidi ya West Ham jana usiku katika robo fainali ya mashindano ya kombe la Carabao.

Arsenal ilifuzu nusu fainali ya mashindano hayo baada ya ushindi huo, huku Danny Welbeck akifunga bao la pekee katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo. Wakati uo huo, Manchester City pia ilifuzu nusu fainali ya mashindani hayo baada ya kuishinda Leicester City kupitia mikwaju ya penalti uwanjani King Power. Baada ya kuchuana na Liverpool, Arsenali itasafiri uwanjani Selhurst Park kuchuana na Crystal Palace, kisha ichuane na West Bromwich Albion. Aidha timu hiyo itachauana na Chelsea uwanjani Emirates katika mechi ya kwanza mwa ujao.