Ole Ntutu Apinga Mswada wa kijinsia

Mbunge wa Narok Magharibi Patrick ole Ntutu amepinga vikali utekelezaji wa mswada kuhusuA� thuluthi mbili ya uwakilishi wa kijinsia na badala yake amependekeza mswada huo kupigiwa kura ya maamuzi . Ole Ntutu amesema iwapo mswada huo utatekelezwa , utaongeza gharama ya mishahara ya wafanyakazi hapa nchini ambayo kwa sasa ni zaidi ya asilimia 50 ya pesa zote zinazotumiwa na serikali . Akiongea katika eneo la Nairashege hukoA� Narok Kaskazini wakati wa mkutano ulioandaliwa katika shule ya msingi ya Medunga��i, Ole Ntutu alisema utekelezaji wa mswada huo utasababisha kutoza ushuru zaidi ili kukimu mishahara yao.

Lakini akiongea katika hafla tofauti mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Narok Soipan Kudate alitofautiana na Ole Ntutu kuhusu swala hilo akisema ni katibu ndiyo inayofafanua swala hilo. Soipan alikuwa akiongea katika shule ya upili yaA� Ntimama ambapo alitoa msaada wa tangiA� ya maji na kutoa hundi kwa wanawake.