Ole Kaparo akejeli mswada uliowasilishwa kwenye bunge la kaunti ya Kiambu

Mwenyekiti wa tume ya kitaifa kuhusu uwiano na mshikamano, Francis Ole Kaparo amekejeli mswada uliowasilishwa kwenye bunge la kaunti ya Kiambu wa kuwashinikiza wenye taasisi na biashara kuhakikisha kuwa asilimia 70 ya waajiriwa ni wakazi wa kaunti hiyo. Kwenye kikao na wanahabari, Kaparo aliwataka waakilishi wa bunge hilo kutupilia mbali mswada huo akisema unakiuka katiba. Alisema wakenya wana haki ya kuishi na kufanya kazi mahali popote humu nchini wa sio kwenye kaunti walikozaliwa pekee.Kaparo aliwahimiza Wakenya kushiriki kwenye shughuli zinazohimiza uwiano wa kitaifa akisema tume hiyo itaendelea kushinikiza utekelezaji wa sheria kuhusu uwiano na mshikamano wa kitaifa.