Ofisi Za Wakili Wa Amama Mbabazi Zateketezwa Uganda

Ofisi mbili za mawakili wanaomuakilisha aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi katika kesi yake kupinga ushindi wa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi uliomalizika zimeteketezwa usiku wa kuamkia leo.

Mohamed Mbabazi, wakili anayeongoza mawakili wengine katika kesi hiyo ya Mbabazi, amesema vipakatilishi, tarakilishi na nyaraka zilichukuliwa kutoka ofisi yake.

Afisa mmoja wa ulinzi alipigwa na watu walioivamia ofisi hiyo.

Ofisi nyengine iliyoingiliwa ni ya wakili Fred Muwema.

Polisi Uganda wanasema wanafanya uchunguzi.