ODM Yafanya Mkutano Kukomesha Mivutano Chamani Humo

Viongozi wa chama cha ODM kwa sasa wako kwenye mkutano unaolenga kukomesha mivutano chamani humo. Katika siku za hivi punde, chama cha ODM kimekumbwa na mtafaruku kuhusiana na suala la demokrasia chamani humo huku baadhi ya viongozi wakihimiza kuondolewa kwa katibu mkuu Ababu Namwamba na naibu mwenyekiti wa chama hicho Paul Otumo ambao wanaonekana kuegemea mrengo wa Jubilee. Namwamba na Otuoma wanahudhuria mkutano huo. Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga alisema kwenye mkutano mjini Busia kuwa wabunge wanaoonekana kuwa waasi watapewa nafasi ya kutoa maoni yao ambayo yatashughulikiwa. Raila alisema Namwamba na Otuma bado ni wanachama wa chama cha ODM na akawahimiza viongozi wengine kudumisha demokrasia. Namwamba na Otuoma wamekuwa wakilalamika kuwa wanatengwa wakati wa kufanya maamuzi muhimu chamani humo.