ODM kurejelea uteuzi wa kuwania ugavana kaunti ya Busia kufuatia kasoro zilizoripotiwa

Chama cha ODM kimefafanua kwamba kitarejelea uteuzi wa kuwania ugavana wa kaunti ya Busia katika maeneo bunge ya Teso-kaskazini na Teso kusini pekee mnamo tarehe 25 mwezi huu. Bodi ya taifa ya uchaguzi ya chama cha ODM inasema kasoro ziliripotiwa katika maeneo bunge hayo mawili huku matokeo ya maeneo bunge yaliosalia yakiwa ya kuridhisha. Akiongea katika makao makuu ya chama cha ODM , mwenyekiti wa bodi hiyo, Judith Pareno, alisema chama hicho kimewabadilisha maafisa wa uchaguzi waliosimamia uteuzi huo uliokumbwa na utata. Pia aliwahimiza wawaniaji kuzingatia agizo hilo jipya la bodi hiyo.

Tangazo hilo limetolewa huku mbunge wa Funyula Paul Otuoma akitishia kususia marudio ya uteuzi huo. Otuoma badala yake amekitaka chama hicho kumkabidhi cheti cha uteuzi wa kuwania ugavana wa Busia. Aidha anataka gavana Sospeter Ojaamong kuto-ruhusiwa kushiriki kwenye kinyanga��anyiro hicho. Mbunge huyo wa Funyula alipata kura 63,752 dhidi ya kura 92,358 za gavana Ojaamong tangazo lililozua maandamano miongoni mwa wafuasi waA� Ojaamong.