Obama- utulivu Nchini Syria

Rais Barrack Obama wa Marekani amesema kuwa majuma kadhaa yajayo yatakuwa muhimu kwa mstakabali wa taifa la Syria kabla ya kuanza mazungumzo ya wiki mbili ya kujaribu kurejesha hali ya utulivu nchini humo.

Obama aliionya Russia kuwa pande zote husika zinapaswa kusitisha mashambulizi yakiwemo yale ya angani.

Aliongeza kuwa ufanisi wa kuafikiwa kwa mkataba wa kusitisha mapigano utategemea iwapo pande zote husika zikiwemo serikali ya Syria, Russia na washirika wao zitajitolea kuheshimu makubaliano hayo.

Alisema kuwa mashambulizi hayo yanapaswa kusitishwa na misaada ya kibanadamu kupelekwa kwa raia wanaoteseka.