Nyong’o ashinda kesi ya uchaguzi dhidi yake

Kulikuwa hali ya msisimuko nje ya mahakama kuu mjini Kisumu jana baada ya jaji David Majanja kutupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na gavana wa zamani wa kaunti ya Kisumu Jack Ranguma kupinga kuchaguliwa kwa gavana wa sasa,A�profA�A�Anyanga�� Nyonga��o. Jaji Majanja alitupilia mbali madai ya Ranguma yakiwemo yale ya wizi wa kura na kutojumuishwa kwa matokeo katika vituo vitano vya kupigia kura. Kulingana na Jaji Majanja, matokeo kutoka vituo hivyo vitano hayangeweza kubadili matokeo ya uchaguzi huo. Aidha aliyataja madai yaliyotolewa na gavana huyo wa zamani kwenye kesi hiyo kuwa yasio na msingi na ya kufedhehesha kwani hakukuwa na ushahidi wa kuthibtisha madai ya kuvurugwa kwa uchaguzi.

Ranguma ameamuriwa kulipia gharama ya kesi hiyo ya shilingi milioni-5 zitakazogawanywa kati ya Nyonga��o na tume ya IEBC.A�Nyonga��o alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo baada ya kuzoa kura 227,127 dhidi ya kura 156,963 za Ranguma.