Nyadhifa Za Makamishna Wa IEBC Zatangazwa

Nyadhifa za mwenyekiti na makamishna wapya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka sasa zimetangazwa rasmi kuwa wazi. Jopo la uteuzi wa makamishna hao limetoa wito kwa wakenya waliohitimu kutuma maombi ya kazi kabla ya tarehe saba mwezi ujao. Kupitia tangazo kwenye magazeti ya humu nchini, jopo hilo limekariri kwamba wanaowania wadhifa wa mwenyekiti ni sharti wawe na shahadaA� kutoka chuo kikuu kinachotambulika, wawe na ujuzi katika maswala ya uchaguzi, usimamizi, fedha, sheria na pia wanaweza kuhudumu kama jaji katika mahakama ya juu. Pia lazima wawe na ujuzi wa kazi wa miaka 15. Aidha, wanaowania nyadhifa za makamishna wa tume hiyo ya IEBC lazima wawe na shahada kutoka chuo kikuu kinachotambulika pamoja na ujuzi katika maswala ya uchaguzi, fedha, usimamizi na sheria.