Nwanko Kanu Aimiza Taifa Hili Kukuza Talanta Za Watoto Wanaopenda Soka

Gwiji wa Nigeria Nwanko Kanu amesisitiza kuwa ni muhimu kwa taifa hili kukuza talanta za watoto wanaopenda soka.

Kanu, alikuwa akizungumza wakati wa mazoezi ya watoto wenye umri wa miaka 13 katika shule ya upili ya Eastleigh. Mshindi huyoA� mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora Barani Afrika Nwanko Kanu, amesisitiza umuhimu wa kuwapo kwa shule za kuwafunza watoto soka humu nchini kwasababu ni watoto hao watakaoipeperusha bendera ya taifa hili na bara Afrika katika siku za usoni.

Kanu, aliyetwaa taji ya ligi ya vilabu bingwa Barani Ulaya akiichezea timu ya Ajax ya Uholanzi, aliwahimiza wadau kuunga mkono juhudi za kukuza talanta za soka nchini Kenya na Barani Afrika, huku akiwasihi wachezaji wa Afrika wanaocheza soka ya kulipwa nga��ambo kuwa mfano bora kwa watoto wanaowaiga.

Nyota huyo aliyeichezea Arsenal awali alifanyiwa upasuaji wa moyo mwezi November mwaka 1996 alipokuwa mchezaji wa Inter Milan, na atatembelea hospitali kuu ya Kenyatta kwa mujibu wa wakfu wake.

Aidha, Kanu ni mmoja wa kikosi cha Arsenal, almaarufu a�?the invinciblesa�� kilichomaliza msimu wa mwaka 2003/2004 wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza bila kushindwa mechi hata moja.