NTSA Kununua Vifaa Zaidi Kuhakikisha Usalama Barabarani

Wakenya wamehimizwa kuwa waangalifu barabarani na kuhakikisha madereva wa magari ya uchukuzi wa abiria yanaendeshwa vyema ili kuhakikisha maisha zaidi hayapotezwi kupitia ajali za barabarani.Akiongea wakati wa siku ya dunia ya kuwakumbuka waathiriwa wa ajali za barabarani, mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya kitaifa ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA Francis Meja, alisema ajali nyingi kwenye barabara za hapa nchini zinaweza kuzuiwa iwapo madereva watakuwa waangalifu na kuwajibika.Aliwahimiza abiria kuhakikisha madereva wanaendesha magari kwa uangalifu na kukoma kuwapongeza wanapovunja sheria za usalama barabarani.Wakati huo huo , Meja alisema halmashauri hiyo itanunua vifaa zaidi zikiwemo kamera za kupiga picha usiku ili kuwapam maafisa wake uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu yao ya kuhakikisha usalama barabarani.Alisema masaa hatari zaidi ni ya usiku kwasababu kwa wakati huu halmashauri yake haina vifaa vya kunasa kasi ya magari gizani.