Nkaissery Akanusha Madai Ya Raila Kuhusu Unyanyasaji Wa Machifu

Waziri wa usalama wa kitaifa meja mstaafu Joseph Nkaiserry amepuuzilia mbali madai ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa amekuwa akiwanyanyasa machifu kuhusiana na shughuli ya usajili wa wapiga kura.Kwenye taarifa Nkaissery alisema kuwa madai hayo ya Raila si kweli na kwamba ni uzushi wa kisiasa tu.Alisema maagizo ambayo amekuwa akitoa kila wakati yanakusudiwa kuhakikisha kuna utengemano na uzingatiwaji wa sheria ili kuwawezesha wahusika kutekeleza majukumu yao ipasavyo.Raila alidai kuwa Nkaissery anatumiaA� mamlaka yake kuwatisha machifu,hasa wale ambao hawataiunga mkono serikali wakati huu wa usajili wa wapiga kura.