Nkaissery aelezea mikakati ya serikali kuhusu usalama nchini

Waziri wa usalama wa kitaifaA� Joseph Nkaissery amesema serikali imeweka mikakati ya kutosha ya kushughulikia tatizo la utovu wa usalama katika maeneo yanayokumbwa na machafuko hapa nchini. Mikakati hiyo ni pamoja na kupelekwa kwa maafisa zaidi wa polisi , operesheni kali za kutwaa silaha zinazomilikiwa kiharamu na kuharibiwa kwa silaha zinazomilikiwa kiharamu .Kwenye taarifa waziri amesema serikali pia imechapisha katika gazeti rasmi la serikali kaunti zaA� Baringo na A�Laikipia kama maeneo yanayokumbwa na machafuko ili kuimarisha zaidi operesheni za usalama katika maeneo hayo. Vile vile Nkaissery amesema serikali imeanzisha juhudi za uhamasishaji kupitia makongamano mbali mbali na viongozi wa maeneo husikaA� ili kuhamasisha wananchi dhidi ya kuvamia ardhi za umma na za kibinafsi. Aidha amesema wale waliokamatwa kwa kuvamia mashamba ya kibinafsi wameshtakiwa. Kadhalika ilani imetolewa ya kusimamisha ukodishaji upya wa ardhi hasa katika ardhi ambazo muda wao wa kukodishwa umekamilikaA� .A� Serikali pia imehimiza mazungumzo kati ya kamati ya usalama na ujasusi katika maeneo ya kaunti na wamiliki wa mashamba na jamii za maeneo husika ili kukuza amani miongoni mwao.