Nkaisserry aonya wawaniaji dhidi ya kuchochea fujo kwenye chaguzi za mchujo

Serikali inashirikiana na tume huru ya uchaguzi na mipaka kuhakikisha kuwa wawaniaji wanaochochea au kuzua fujo kwenye chaguzi za mchujo zinazoendelea wamepigwa marufuku kushiriki kwenye uchaguzi. Waziri wa usalama Joseph Nkaisserry amesema tayari wawaniaji wawili wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali kuhusiana na vitendo vya kihalifu, akiongeza kwamba hatua zitachukuliwa dhidi ya wanaovuruga amani.A�A� Akiongea na wanahabari jijini Nairobi jana, Nkaissery alisema serikali imejitolea kudumisha amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti. Alitaja kaunti za Homa Bay, Kisii, Migori, Kisumu, Busia, Bungoma, Kiambu, Muranga��a, Nakuru, Kajiado, Embu na Mombasa kuwa maeneo ambayo yameshuhudia ghasia za kisiasa katika siku za hivi punde. Aidha Nkaissery aliwaonya maafisa wa usalama watakaoegemea pande fulani kwenye uchaguzi wa mchujo kwamba wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Aliwahimiza wakenya wadumishe amani wakati wa chaguzi za mchujo huku akiwataka maafisa wanaosimamia chaguzi hizo kuwajibikia usalama na utulivu katika vituo vya kupigia kura.