Nkaiserry ataja baadhi ya sehemu za Baringo kuwa hatari

Waziri wa usalama wa kitaifa Joseph Nkaiserry ametaja sehemu fulani za kaunti ya Baringo kuwa hatari. Hii inafuatia agizo lililotolewa na naibu wa rais William Ruto, alipozuru kaunti hiyo Jumatatu wiki hii. Maeneo hayo yaliyotangazwa kupitia gazeti rasmi la serikali kuwa yaliyo na wasiwasi yasiyokuwa salama kwa kuishi ni pamoja na Arabal, Kiserian, Mochongoi, Rugus ,Mukutani, Chebinyiny, Komolion, Chepkalach, Makutano, Paka ,Orus, Loiywat, Silale ,Nando, Tangulbei, Chepkererat, Kipnai, Ng’oron na Amaya. Arifa hiyo inayoyoweza kuondolewa au kuongezwa muda, itatekelezwa katika siku 30 zijazo huku misako ya kiusalama ikiendlea katika sehemu hizo. A�