Njia Mpya Ya Kuadimisha Chanjo Ya Polio Yaidhinishwa

Mbinu ya utoaji chanjo ya ugonjwa wa kupooza kupitia mdomo hapa nchini itabadilishwa na chanjo ya kutolewa kupitia sindano kufikia mwezi Aprili mwaka huu. Kaimu mkurugenzi wa huduma za matibabu Dr. Jackson Kioko amesema Kenya imepiga hatua kubwa kwa kuidhinisha mbinu hiyo. Dr. Kioko amesema chanjo hiyo itatolewa mara moja kwa mwaka tofauti na ile ya kutolewa kupitia mdomo iliyokuwa ikitolewa mata tatu kwa mwaka. Akiongea wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa chanjo hiyo mjini Muranga��a ,Kioko amesema baadhi ya dozi za chanjo ya kutolewa kupitia mdomo zilihusishwa na visa vya watu kulemazwa. Alisema chanjo hiyo itawapa kinga watoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja na iatolewa miongoni mwa chanjo nyingine zilizoko.