Nigeria yapeleka vikosi zaidi kuwasaka wanafunzi 110 wa kike waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram

Nigeria imepelekaA�A�vikosi zaidi vya kijeshi pamoja na ndege kuwasaka wanafunzi wa kike 110 wanaoaminika kutekwa nyara na kundi la wanamgambo la book haram wiki iliyopita . Wasichana hao walipotea baada ya wanmagmabo hao kuvamia shule yao katika mji wa Dapchi uliko Kaskazini Mashariki mwa jimbo la Yobe . RaisA�A�Muhammadu Buhari alisema kuwa ni makasa wa kitaifa na kuomba radhi kwa familia za wasichana hao. Shambulizi hilo limefufua kumbukumbu za kutekwa nyara kwa wanfaunzi wa kike wa shule ya Chibok mnamo mwakaA�A�2014.

Jamaa waliokuwa na ghadahabu walitaka majibu kutoka kwa serikali huku kukiwa na ripoti kuwa wanajeshi waliondolewa kutoka kwa maeneo muhimu ya ukaguzi wa kiuslama mjini humo mwezi uliopita. Mji wa Dapchi, umbali wa kilomitaA�A�275 kaskazini magharibi mwaA�A�Chibok, ulishambuliwa Jumatatu iliyopita na kusababisha walimu na wanafunzi kutoka chuo cha mafunzo cha sayansi na kiufundi kukimbilia kichaka kilicho karibu.