Ni Marufuku Kuchati Kazini Tanzania

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewapiga marufuku wafanyakazi wake ”Kuchati” katika mitandao ya kijamii kwa kutumia simu katika muda wa saa za kazi.

Wizara Makame Mbarawa (Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano) amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi, kutumia muda mwingi maofisini kuperuzi katika mitandao ya kijamii pamoja na kupiga porojo, hali inayosababisha kushuka kwa uzalishaji na maendeleo.

Ameongeza kuwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria, na pia kuwataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa na bidii ya kazi na weledi.