Ndoto Ya Kuwa Na Paspoti Ya Bara Africa Inakaribia Kutimia

Ndoto ya kuwa na paspoti ya bara Afrika ambayo itaruhusu usafiri huru barani humu bila haja ya kuwa na hati ya viza inakaribia kutimia kufuatia makubaliano ya viongozi wa nchi na serikali wanachama wa muungano wa Afrika wanaokutana mjini Kigali nchini Rwanda. Ili kufanyia majaribio mpango huo, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Amina Mohammed anasema viongozi wa mataifa ya kiafrika na mawaziri wao wa mashauri ya kigeni watakuwa wa kwanza kukabidhiwa paspoti hiyo na kisha itakabidhiwa raia wengine wa bara hili. Amina alipongeza mwelekeo wa mkutano wa 14 wa umoja wa mataifa kuhusu biashara na maendeleo-UNCTAD kufikia sasa na kuafikiwa kwa malengo muhimu kwenye mkutano huo. Wakati huo huo kuafikiwa kwa malengo ya maendeleo endelevu na mataifa yanayostawi kungali hakujaafikiwa kutokana na changamoto za kifedha. Mataifa yaliostawi kwa sasa yanakabiliwa na uhaba wa dolla trilioni 2 na yanahitaji dolla trilioni 2.5 kwenye uwekezaji wa kila mwaka ili kuafikia malengo la maendeleo endelevu. Balozi Amina anasema mataifa yaliostawi yahitaji kuchunguza njia mbadala za kujiletea mapato kama ushirikiano katika uwekezaji, hazina za malipo ya uzeeni na uwekezaji katika miradi ya muundo msingi kuunga mkono misaada ya kigeni. Mataifa yaliostawi yaliangaziwa kwa kuto-timiza lengo lao la mwaka 2002 la kutenga asimilia 0.7 ya jumla ya mapato yao ya kitaifa kutoa misaada kwa mataifa ya nga��ambo.

A�