Ndoa Ya Jinsia Moja Yamlazimisha Bintiye Askofu Mkuu Desmond Tutu Kuacha Kazi Nchini Afrika Kusini

Bintiye askofu mkuu Desmond Tutu amelazimika kuacha A�majukumu yake ya ukasisi katika kanisa moja la kianglikana nchini Afrika kusini baada ya kusemekana kumuoa mwanamke mmoja nchini humo kwa mujibu wa shirika la habari la A�AFP. A�Kasisi A�Canon Mpho Tutu-van Furth sasa hawezi A�kutekeleza majukumu yake ya ukasisi kwa vile kanisa hilo haliruhusu ndoa za jinsia moja. Alisema kuwa baba yake A�ambaye ni askofu mkuu mstaafu na mwanaharakati mashuhuri wa kupinga ubaguzi wa rangi A�hakufurahia hatua hiyo na lakini pia haikumshangaza. Sheria za kanisa hilo zinasema kuwa ndoa inastahili kuwa baina ya mwanaume na mwanamke. Wawili hao walikuwa wameolewa na kuwataliki mabwana zao licha ya kuwa wana watoto. Ndoa za jinsia moja zilihalalishwa nchini Afrika kusini mwaka wa 2006.