Ndege Za Kivita Za Marekani Zatekeleza Mashambulizi Dhidi Ya Wanamgambo Wa Islamic State, Libya

Ndege za kivita za Marekani zimetekeleza mashambulizi dhidi ya ngome za wanamgambo wa Islamic State nchini Libya,kutokana na ombi la serikali ya nchi hiyo.Habari hizo ni kwa mujibu wa idara ya ulinzi ya Marekani.Mashambulizi hayo yalilenga mji wa bandari wa Sirte,amba ni ngome kuu ya wanamgambo hao.Waziri mkuu wa Libya Fayez Sarraj,kwenye hotuba yake ya runinga kwa taifa hilo ,alisema adui alipata hasara kubwa kufwatia shambulizi hilo.Mataifa ya magharibi yameelezea wasi wasi mkubwa kutokana na ongezeko la wapiganaji wa kundi hilo nchini Libya.Shambulizi hilo la ndege za kijeshi za Marekani ndilo la kwanza la kigeni kushirikishwa na majeshi ya Libya,mbali na yale mawili yaliotekelezwa mnamo miezi ya februari na Novemba mwaka jana.Idara ya ulinzi ya Marekani ilisema kuwa mashambulizi hayo yaliidhinishwa na rais Barack Obama na ni sehemu ya harakati zake dhidi ya wanamgambo wa Islamic State.