NCIC Yaonya Kuhusu Uwezekano Wa Ghasia

Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa A�(NCIC) imetoa tahadhari kuhusiana na taharuki kote nchini na uwezekano wa A�ghasia kuzuka huku nchi hii ikielekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017. Akiongea katika eneo la Chaaria kaunti ndogo ya Imenti ya kati , kamishna A�Adan Mohammed alishtumu machafuko yaliyozuka siku ya Jumatatu wakati wa maadhimisho ya siku ya A�Jamhuri mjini A�Meru na kusema visa vibaya zaidi vinatarajiwa kutokea. Mohammed alisema Kenya imegawanyika kisiasa na kuhimiza pande zote kufanya kampeni zao kwa amani. Alisema tume hiyo inatoa mafunzo kwa maafisa wa upelelezi wa jinai ili kunakili sauti na picha za wanasiasa wanaochochea watu. Matamshi yake yaliungwa mkono na kamishnaA�GitileA�Naituli, aliyesema viongozi wanaendeleza ufisadi na ukabila ambazo ni hatari huku nchi hii ikielekea katika uchaguzi